Simulizi : Nakupenda Cindelela
Sehemu Ya Tatu (3)
Majaribio yalianza huku kocha akiangalia uwezo wa kila mchezaji hasa kwenye suala la kumiliki mpira pamoja na kujituma katika mazoezi ya nje ya uwanja.Kila mtu katika benchi la ufundi alikuwa anafurahia mazoezi yanavyoendelea sababu wachezaji wote walikuwa wanajituma kwa nguvu ili wapate nafasi ya kuchaguliwa katika hayo majaribio
“hawa vijana wanaonekana wanajituma sana mpaka nashindwa nimchague nani na nimuache nani katika haya majaribio”alisema kocha mkuu huku akiangalia wale wachezaji kwa makini jinsi walivyokuwa wanafanya mazoezi binafsi
“Hapa inatubidi tufanye kitu ili kuwachuja hawa wachezaji na tubaki na wachache”alisema kocha msaidizi
“tufanye kitu gain?”aliuliza kocha mkuu
“inatubidi ttutafute mechi ya majaribio baada ya kuangalia uwezo wao kwa hizi siku mbili “alisema kocha msaidizi
“kweli hapa wakimaliza majaribio inabidi tuombe mechi na timu yoyote hata kama ni ya England conference league(ligi iliyokuwa chini ya ligi ya championship na England one)”alisema kocha na wote walikubaliana na lile wazo
Katika majaribio yale Alex alionekana kujituma sana katika majaribio japo hali ya hewa ilikuwa inamzingua kutokana na ugeni aliokuwa nao katika nchi ile ya Uingereza.Alex alikuwa anajituma kwa nguvu zote sababu hakutaka kurudi tena Tanzania kuishi maisha ya dhiki aliyokuwa anaishi hapo hawali kabla ajaja England
“hapa lazima nifanye niwezavyo ili nipite katika majaribio aya”Alex alijisemea mwenyewe huku akizidisha juhudi
Siku ya kwanza ilikatika na wachezaji wakaruhusiwa kwenda kwenye makazi yao ili kesho yake waaanze tena majaribio katika hatua nyingine tena.Alex alipelekwa kwenye chumba chake na kuelekea kuoga kisha akajipumzisha ili kutuliza akili yake kwasababu alikuwa amechoka sana.
Alex alijikuta anapitiwa na usingizi huku akiota ndoto ambayo ilimfanaya ashtuke na jasho zianze kumtoka kwa wingi kama ametoka kufanya mazoezi.Alex aliota hivi
Alikuwa na msichana Cindelela wakiwa wamekumbatiana huku wakicheka kwa furaha sababu hali ya upendo ilikuwa katikati yao.Cindelela alikuwa anamuangalia Alex kwa macho ya kurembua huku akimbusu kwenye mdomo wake mara kwa mara.Moyo wa Alex ulikuwa unasuuzika sababu ile fursa aliyokuwa anaingoja kwa hamu ilikuwa tayari imeshawadia.Alex alikuwa anaonyesha wazi kama kweli anampenda Cindelela sababu macho yake yalikuwa yanaonyesha taswira tosha ya upendo wake kwa Cindelela
“Nakupenda sana Cindelela wewe ndiyo msichana wa maisha yangu sidhani kama atatokea msichana mwingine ambaye atashika akili yangu kama wewe ulivyoishika NAKUPENDA SANA CINDELELA”Alex alisema huku akitaka kumkumbatia Cindelela
“Nakupenda pia”Cindelela alisema
Alex alijikuta akisukumwa kwenye maporomoko na kupiga kelele ambazo zilimuamsha kwenye usingizi.Alex alishtuka na kukaa kitandani huku akijiuliza ni nani aliyemsukuma kwenye ile ndoto sababu Cindelela alikuwa kwa mbali kidogo na mkono ulitokea upande mwingine kisha ukamsukuma kwenye maporomoko
“ni nani aliyefanya hivi?je hii ndoto ni kweli?”Alex alijiuliza huku akitetemeka mwenyewe
Alex hakuwa na hamu tena ya kuendelea kulala sababu aliiogopa sana ile ndoto aliyoota,aliinuka pale kitandani na kwenda kunawa uso wake kisha akatoka nje ili kuangalia mazingira.Alitembea tembea kila maeneo ya pale pale ili kusafisha macho yake.Alipolidhika kutembea tembea aliamua kurudi kwenye chumba chake ili atulie kesho yake aingie kwenye majaribio mengine
Kama ilivyohada majaribio yalifanyika ndani ya siku tatu na makocha walilizishwa na viwango vya wachezaji sababu wote walikuwa wanaonyesha uwezo wa hali ya juu.Uongozi wa timu ukaamua uchague wachezaji sita ambao walifanikiwa kupita katika mchujo wa kwanza.Alex alikuwa ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kupita katika huo mchujo wa kwanza na kukamilisha watu sita ambao nao wanatakiwa wachujwe ili wabaki watatu
Uongozi wa timu uliamua kutafuta timu ambayo wangecheza nayo mechi ili wawapime wale wachezaji sita waliobaki na kuchagua watatu ambao wangeungana na timu yao.Michakato ya kutafuta timu ikaanza na timu waliyoipata kwaajili ya kucheza mechi ya kirafiki ilikuwa inaitwa Forest green ambayo ilikuwa inashiriki England conference league
Kwakuwa walikuwa wachezaji sita ambao kila nafasi walikuwa wachezaji wawili wanaocheza nafasi moja,Katika nafasi ya beki kuliwa na wachezaji wawili ambao mmoja wao alikuwa anatoka Nigeria mwingine ni Cameroon.Katika nafasi ya kiungo nako kulikuwa na wachezaji wawili ambao mmoja alikuwa anatoka Ivory coast na mwingine alikuwa anatoka Chad.Katika nafasi ya ushambuliaji kulikuwa na wachezaji wawili ambapo Alex alikuwa ni mmoja wao na mwingine alikuwa ni raia wa Senegal.Ktika kila nafasi alitakiwa apatikane mchezaji mmoja ambae atajiunga na timu hiyo
Wachezaji hao wote walikuwa ndani ya kikosi kilichokuwa kinacheza siku hiyo huku baadhi ya nafasi nyingine zilijazwa na wachezaji waliokuwa tayari wamesajiliwa na hiyo timu.Alex hakuwa na Pressure sana japo mpinzani wake ambae walikuwa wanacheza katika nafasi moja alionekana kuwa ni moto wa kuotea mbali.Alex alisali kimoyomoyo huku akimuomba mungu wake ili afanye vizuri katika ile mechi ambayo ilikuwa inaanza muda siyo mrefu
Refa alipuliza kipenga na mechi kaanza kwa kasi huku yule raia wa Senegal akionyesha ufundi wa kupiga chenga na kutoa pasi za uhakika.Alex alijitahidi sana kuonyesha uwezo wake kwa kuchukua mipira kati kati na kupiga pasi ndefu ambazo zilikuwa zinawafikia wausika.Haikuishia hapo Alex alikuwa anapiga chenga mabeki hadi watatu na kupiga mashuti ambayo yalikuwa yanaenda langoni ila kwa umahiri wa goli kipa aliweza kuyapangua na kufanya Alex ashindwe kufunga Goli
Upinzani uliokuwa unaonyeshwa na safu ya mbele uliwafanya makocha waanze kusugua kichwa huku wakifurahi kimoyomoyo sababu upinzani ulikuwa mkali kuliko kwenye nafasi nyingine.yule raia wa Senegal alifanikiwa kufunga goli ambalo liliwafanya makocha wasimame na kuanza kumshangilia kwa goli alilolifunga.Hawakujua kama kile kitu kilimuumiza sana Alex na kujiona kama anaikosa ile nafasi ya kuchaguliwa
Kipindi cha kwanza kiliisha na wachezaji wakaenda kuongea na kocha mambo mawili matatu ili wakirudi kipindi cha pili wabadilike.Walirudi uwanjani kwaajili ya kipindi cha pili huku Alex akianza kukata tama kutokana na lilegoli alilolifunga mwenzake lilimkosesha rha na kuona kama ile nafasi ingempotea
Kipindi cha pili kilianza na Alex alianza kuonyesha vitu vyake sababu alishajiapia kwamaba hataki tena kurudi Tanzania.Alex alipata pasi kutoka kwenye upande wa kushoto na kuanza kuingia nao katikati huku akipiga chenga mabeki,alitoa pasi safi sana ambayo ilirudihwa kwake tena kisha akapiga shuti kali ambalo liliingia moja kwa moja golini
Watu walishangilia na kufanya Alex apate moyo wa kuendelea kufanya mambo mazito uwanjani mpaka makocha wakaanza kukuna vichwa vyao sababau ilikuwa ni utamu wa hali ya juu.Dakika ya themanini na tisa Alex aliipatia timu yake bao la baada ya kuwapunguza wachezaji watatu kwenye boksi na kupiga mpira kwa shuti la taratibu sana lakini ukaingia wavuni sababu aliupiga kiufundi
Mpira uliisha na wachezaji walitoka uwanjani huku Alex akionyesha furaha ya ajabu sababu alifanya vile inavyotakiwa.Kocha aliwachukua wachezaji wote na kuelekea nao chumba cha kubadilishia nguo.Wachezaji waliingia bafuni na kuoga kwaajili ya kubadilisha nguo na waende kupumzika kwenye vyumba vyao
“kesho ndiyo tutatangaza nani anabaki na sisi katika timu yetu”kocha Aliwaambia wachezaji wake baada ya kutoka kuoga
Wachezaji wote walielekea kwenye vyumba vyao kwaajili ya kupumzika.Kichwani mwa Alex alikuwa anawaza kama nay eye atabaki katika hiyo timu au atarudi nyumbani.Japo alicheza vizuri lakini hakutaka kujihakikishia moja kwa moja kama atabaki katika club hiyo.Alex alijipumzisha kitandani baada ya kula ili kesho akasikilize mmatokeo ya mchujo
Kesho yake asubuhi wachezaji wote waliitajika katika chumba cha mikutano kwaajili ya kutangaza wachezaji amabao watabaki katika timu hiyo.mwenye Mr Peter Pannu alisimama na kushika karatasi ambayo ilikuwa na majina ya wachezaji ambao wamechaguliwa na uongozi wa club.
“haya ndiyo majina ya wachezaji ambao watabaki kwenye club yetu na ndio tutasign nao mkataba muda siyo mrefu kuanzia sasa.Nafasi ya beki ni Jonathan,Nafasi ya kiungo ni Lucas kutoka Chad,na katika nafasi ya ushambuliaji ni Alex kutoka Tanzania”Peter Pannu alisema na kufanya Alex masikio yake yazibuke sababu yalikuwa yameziba kwa muda mrefu
“Leo tutasign mikataba kwaajili ya kuanza mazoezi hapo kesho “alisema Peter Pannu
Walikabidhiwa mikataba yao na kuanza kuisoma huku waandishi wa habari wakichukua picha kwaajili ya kuzirusha kwenye vyombo vyao.Katika mkataba wa Alex alikutana na kipengelea ambacho kilimruhusu kusoma huku akiendelea na mpira.mkataba wake ulimfanya awe anapokea paund elfu tano ambayo ni sawa na million kumi na mbili ya kitanzania huku akihaidiwa kusomeshwa bure katika chuo cha Birmingham university
Alex alifurahi sana kupata ile nafasi ya kusoma huku akiendelea kucheza mpira katika club ile.Alex alipewa mkataba wa miaka mitano kwaajili ya kuitumikia club ile huku akiendelea kusoma.Alex aliambiwa atakaa kwenye nyumba za kawaida na wenzake mpaka pale atakapotafutiwa makazi yake binafsi
“Asante sana mungu kwani umenitendea miujiza”alex alijisemea mwenyewe huku akiweka sign katika ule mkataba
Walimaliza kila kitu na wachezaji wote wakarudi kwenye vyumba vyao kwaajili ya mapumziko wa wiki moja ndiyo wajiunge na wachezaji wenzao kwaajili ya kuanza mazoezi rasmi.Uongozi wa timu nao ulikuwa unafuatilia chuo cha Birmingham ili Alex ajiunge nacho kwaajili ya masomo yake
Siku zilikatika na Alex akaanza rasmi mazoezi katika timu ya Birmingham city huku akiendelea na masomo katika chuo cha Birmingham university.Alex alikuwa anajitahidi sana kuzingatia masomo yake huku akiendelea kucheza mpira katika timu yake japo ligi ilikuwa bado haijaanza ila walikuwa wanacheza mecho za kirafiki ili kukiimarisha kikosi chao pindi ligi itakapoanza
Katika kipindi kifupi Alex alianza kupata umaarufu hasa pale chuoni kwao sababu alikuwa anapenda sana kushiriki katika mechi zinazohusu chuo chao na chuo kingine.Alex alikuwa anaonyesha soka safi kiasi kwamba hata wanafunzi wa pale chuoni walikuwa hawaamini kama kuna mswahili anaweza kucheza mpira kiasi kile sababu walikuwa wanawadharau sana waafrika kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo
Taratibu Alex alianza kupata marafiki mbalimbali ambao walikuwa wanapenda tu kuwa nae sababu alikuwa ni mtu wa kujituma katika masomo pamoja na Mambo yake ya mpira.Marafiki wengi aliowapata Alex walikuwa ni wazungu huku waswahili nao wakiwa kwa wingi.Alex alianza kujizolea umaarufu pale chuoni na kufanya watu wengi wawe wanamfuata kila anapokuwepo
Msimu wa ligi ulipoanza Alex alikuwa anaonyesha cheche katika kila mechi aliyokuwa anapangwa kiasi kwamba viongozi wote wakawa wanampenda na kumuhaidi kumuongeza mshahara pindi atakapoendelea kufanya vizuri kataka michezo atakayokuwa anapangwa.Alex aliendelea kufanya juhudi kiasi kwamba muda mwingine alikuwa anakosa nafasi ya kujisomea kutokana na mazoezi makali aliyokuwa anafanya.Hela aliyokuwa anaipata alikuwa anawatumia wazazi wake ili wajenge nyumba kwaajili ya kuboresha makazi yao
Kutokana na uchezaji wake wa kujituma watu wa kwenye jiji la Birmingham wlianza kumfahamu na kumfuatilia katika sehemu alizokuwa anaenda kutembelea wakati wa mapumziko.Watu wengi walikuwa wanamfuata na kutaka sign yake katika nguo zao diary,kofia ba vitu mbalimbali.Alex hakuwa na hiyana alifanya vile watu walivyokuwa wanataka sababu hakupenda kitu kinachoitwa maringo
Kama unavyojua mtu ukiwa na umaarufu lazima kuna wasichana ambao watakuwa wanakusumbua hasa watakapopata namba yako ya simu au Email yako.Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Alex,Alex alikuwa anapigiwa simu na wasichana mbalimbali wakimtaka kimapenzi lakini Alex alikuwa anakataa sababu alikuwa hataki kuchanganya mapenzi na mpira.Kati ya wanawake ambao walitokea kumpenda Alex alikuwa ni Angel
Angel alikuwa ni binti wa mfanya biashara tajili katika nchi ya Ujerumani.Yeye aliamua kushi Uingereza kutokana na masomo ambayo alikuwa anasoma katika chuo alichokuwa anasoma Alex.Angel alikuwa anaemia sana kila alipokuwa anamuona Alex akiwa amesimama na msichana mwingine katika chuo icho.Machozi yalikuwa yanamtoka kila alipokuwa anamuona Alex akikumbatiwa na wadada huku wenine wakiwa wamemzunguka
Alikuwa muoga sana kumfuata Alex na kumueleza ukweli kwamba anampenda kutoka moyoni.Alikuwa hajui aanzie wapi ili aweze kupata nafasi ya yeye kuwa na Alex japo hata kwa usiku mmoja tu.Kingine kilichokuwa kinamuumiza kichwa ni kutokana na lugha aliyokuwa anaitumia ya kijerumani Alex asingeweza kuelewa sababu Alex alikuwa anajua kingereza na Kiswahili tu.Angel aliamua atafute rafiki ambae anaelewa lugha ya kijerumani na Lugha ya kiingereza ili pindi atakapopata nafasi ya kuongea na Alex amtafsilie ili waweze kuelewana
Siku moja Alex akiwa anapata chakula cha mchana ndani ya canteen iliyokuwepo pale chuo.Angel aliamua kumfuata Alex pale alipokuwepo huku akiwa ameongozana na mtafsiri wake.Walifika mpaka kwenye meza aliyokuwepo Alex na kusimama wakisubiri wakaribishwe
“V geit es dia(habari yako)”Angel alisalimia kwa kijerumani
Alex alikodoa macho asijue nini ajibu mpaka pale makalimani wa Angel alipomtafsiria na kufanya Alex atabasamu kisha akajibu kwa kiingereza kwamba sijambo
“es geit mia gut(sijambo)”mkalimani alimjibia Alex
Maongezi yaliendelea bila Angel kuzungumza neno lolote kuhusu mapenzi zaidi ya kumuuliza maswali tofauti kuhusu maisha yake.Alex alikuwa anajibu maswali kutokana na alivyokuwa anaulizwa yale maswali.Angel alijitahidi kuficha hisia zake lakini mwisho wa siku aliamua kusema ukweli ambao ungemuweka huru na maisha yake
“Ish libe dish zozea Alex(nakupenda sana Alex)”Angel alisema na kumuacha Alex akimshangaa sababu akuelewa nini alichosema Angel mpaka pale alipotafsiriwa
Alex alitabasamu sababu kwa kipindi hicho alishazoea kuambiwa maneno kama hayo na wasichana tofautitofauti.Alisugua kichwa chake na kutoa jibu moja tu kwamba anahitaji muda mwingi wa kufikiria kabla ya kutoa maamuzi ya moja kwa moja.Walimaliza kuongea na Angel akaondoka huku wakimuacha Alex akiendelea kula chakula chake
Mwaka mmoja ulikatika bila ya Alex kukubali kuwa na msichana yoyote ndani ya chuo au nje ya hicho chuo.Kipindi cha uchaguzi wa chuo kilifika huku watu wengi wakimuimiza Alex agombanie nafasi ya uraisi sababu alikuwa na watu wengi sana waliokuwa wanampa support na walimuhaidi kama akigombea lazima watafanya juu chini mpaka ashinde nafasi hiyo
“Alex watu wanakupenda sana na ukigombania sidhani kama kutakuwa na mpinzani”Alisema Rafiki yake ambae alikuwa na asili ya Kenya
“sidhani kama inawezekana”Alex alisema
“kwanini isiwezekane?”rafiki yake aliuliza
“nadhani unajua kwamba mimi nina majukumu mengi ndani ya timu na ukicheki mimi bado ni mwanafunzi”alex alisema kwa utulivu
“unajua kwamba ukiwa raisi wa chuo ni jambo la heshima sana?”rafiki yake alimuuliza
“najua ila nitakuwa na mzigo mkubwa sana sidhani kama nitaweza kuhudumia kote”Alex alisema
“Alex mimi nakushauri ugombanie arafu utakuja kuniambia matokeo yake hapo baadae”rafiki yake alisema
“basi ngoja nikachukue form ya uongozi ofisini”Alex alisema na kuelekea ofisini kuchukua form
Watu waliposikia nia ya Alex kugombea uraisi wa chuo walifurahi sana na kuanza maandalizi ya kampeni kwaajili ya kuhakikisha anafanikiwa kushinda katika hiyo ngazi kubwa hapo chuoni.Japo uongozi wa timu ulikuwa unaweka ngumu kwa Alex kugombania nyazfa hiyo lakini baadae walilegeza kamba baada ya ushawishi wa hali ya juu uliofanywa na watu waliokuwa wanamsupport Alex
Kampeni zilianza huku Alex akionekana kukusanya wanafunzi wengi kuliko wapinzani wake kitu kilichofanya kuwanyima raha wale wapinzani.Kila sehemu zilikuwa zimebandikwa picha zilizoandikwa VOTE FOR ALEX huku zikikiwa na picha ya Alex.Hata wanafunzi waliokuwa wanakuja kuchukua form kwaajili ya kujiunga na chuo icho walikuwa wanashangaa kuona watu wengi wakiwa kwenye makundi huku wakiwa wamevaa t shirt zilizokuwa na picha ya Alex
……………………………………………………………………………………………………………………………
Cindelela alikuwa ameshamaliza kidato cha sita na kufahulu vizuri katika masomo yake kitu kilichomfanya baba yake amuambie kwamba achague zawadi yoyote anayoitaka
“mwanangu hongera sana kwa kufahuru masomo yako naomba uchague zawadi yoyote unayotaka nitakupatia”Mzee Jacobo alimuambia mwanae
“baba mimi zawadi yoyote unaweza ukanipatia sababu nashindwa nichague ipi”Cindelela alimuambia baba yake
“mwanangu chagua nchi yoyote unayotaka kwenda kusoma sitaki usome tena Tanzania”Baba yake alisema
“baba unanipa wakati mgumu sana”Cindelela alisema
“wakati mgumu gani niliokupa mwanangu?”mzee Jacobo aliuliza
“mimi sivielewi vyuo vya nje labda unitajie wewe mwenyewe”Cindelela alisema
“kuna rafiki yangu mmoja ni lecture katika chuo kimoja kilichopo Uingereza sema sikumbuki ni chuo gani anachofundisha labda nimtafute arafu nimuulize”Mzee jacobo alisema huku akitoa simu yake kwenye mfuko
Alibonyeza bonyeza simu yake kisha akaweka sikioni ili kusikiliza kama itaita,alianza kutabasamu baada ya kusikia ile simu inaita na kupokelewa
“hallo”mzee Jacobo alisema
“hallo Mr Jacobo za siku nyingi”sauti ya upande wa pili ilisikika
“salama mr Steven,kuna jambo nataka nikuulize”alisema Mr Jacobo huku Cindelela akiwa amemkodolea macho
“niulize tu ndugu yangu”alisema Mr Steven
“hivi wewe ni lecture katika chuo gani?”aliuliza mr Jacobo
“mimi ni lecture katika chuo cha Birmingham university”Alisema Mr Steven
“okey si naweza kumleta mwanangu huko?”mr Jacobo aliuliza
“unaweza ukamleta tena kipindi hiki ndiyo kizuri sababu ndiyo watu wanaingia kama unataka kumleta inatakiwa ufanye haraka”Alisema Mr Steven
“mwanangu anataka kusomea Life and environment science,je inapatikana hapo?”aliuliza mr Jacobo
“ndiyo inapatikana hapa”alisema Mr steven
“basi ngoja nifanye maandalizi ya haraka sana ili nimlete”mzee Jacobo alisema
“okey fanya hivyo”Mr Steven alisema
“okey kwaheri”alisema Mr jacobo na kukata simu
Mzee Jacobo alimgeukia Cindelela na kumuambia kila kitu walichoongea na mr Steven.Cindelela alifurahi sana kusikia kwamba anahitajika kwenda Uingereza kwaajili ya masomo.Alimkumbatia baba yake na kumbusu sababu hiyo ilikuwa zawadi tosha kwake
Safari ilianza kuandaliwa na kwakuwa mzee Jacobo alikuwa ni waziri wa mambo ya nje wala haikuchukua muda mrefu kupata vibali.Kabla Cindelela ajaondoka alimuhaga rafiki yake kipenzi Wit huku machozi yakimtoka sababu walikuwa na urafiki mkubwa sana na kutengana kwao ilikuwa ni jambo la kusikitisha sana
“Wit my dia tutaonana mungu akipenda”Cindelela alisema huku akimkumbatia rafiki yake
“safari njema kipenzi changu tutakuwa tunawasiliana”Wit alisema
Cindelela aliwakumbatia wazazi wake na kuanza kuelekea sehemu ya kupandia ndege sababu muda ulikuwa umeshawadia.Kichwani alikuwa na uzuni sana sababu hakuzoea kuwa mbali na wazazi wake na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kutengana na wazazi wake.Ndege ilianza kuachia ardhi ya Tanzania na kupotelea kwenye mawingu
Ilichukua masaa mengi sana kuwa hewani kitu kilichomfanya Cindelela awe analala kila saa sababu ya uchovu wa kukaa sehemu moja.Walifika nchini Uingereza salama bila misukosuko yoyote angani.Aliposhuka tu uwanja wa ndege watu walandaliwa kwaajili ya kumpokea walimfuata na kubeba mizigo yake na kuingia kwenye gari na safari ya kuelekea hotelini ikaanza
Cindelela alikaa hotelini kwa siku mbili bila kufanya jambo lolote sababu ya uchovu aliokuwa naos.Kila kitu kuhusu chuo alikuwa anakishughulikia Mr Steven ambae ni rafiki wa baba yake.Kazi kubwa ya Cindelela ilikuwa ni kulala na kuangalia movie kwenye chumba chake
Siku ya kuanza chuo iliwadia na Cindelela akawa ndani ya gari la Mr steven wakiwa wanaelekea chuo kwaajili ya kuanza masomo yake.Macho yake yalikuwa yanaona makaratasi yakiwa yamebandikwa ukutani huku yakiwa yameandikwa VOTE FOR ALEX lakini picha alikuwa anashindwa kuiona sababu gari lilikuwa linatembea.Pia alikuwa anawaona watu wengi wakiwa wamevaa nguo zilizoandikwa neno ilo
“Samahani Alex ni nani?”Cindelela aliamua kuvunja ukimya na kuuliza swali
“ni mwanafunzi mmoja hivi anagombania uraisi wa wanafunzi ila anaonyesha kwamba atashinda sababu kila mtu anampenda”alijibu mr Steven
“basi inaonekana ana nyota ya ushawishi sana natamani hatannimuone”Cindelela alisema bila kujua kama Alex ndo yule aliyekuwa nae Tanzania
“Usijali kwa umaarufu aliokuwa nao lazima utamuona tu”Mr Steven alisema huku akiegesha gari
Walishuka kisha safari ya kuelekea ofisini ikaanza ili wakakamilishe usajili na Cindelela aanze masomo.Walifika ofisini na taratibu zote zilifuatwa kisha Cindelela akapelekwa kwenye darasa(lecture room) ambalo atakuwa anasomea kila siku.Japo ilo darasa lilikuwa na wanafunzi wapya lakini midomoni mwao walikuwa wanazungumza kuhusu Alex
“Alex lazima atashinda uchaguzi sababu watu wengi wanaonekana kumpenda”alisema mwanafunzi mmoja wa kizungu akimuambia mwenzake
“hiyo ni kweli na kwa jinsi alivyo handsome tena mweusi natamani hata niwe nae sababu na mimi nitakuwa maarufu”Alisikika mwanafunzi mwingine akisema
Kwa jinsi mazungumzo yalivyokuwa yanaendelea ndiyo kiu ya Cindelela kumjua Alex iliongezeka maradufu. Sabababu Alex alionekana ni mtu mweusi arafu ni maarufu sana wakati kitu icho kilikuwa ni kigumu sana kutokea katika nchi za ulaya.Cindelela aliendelea kusikiliza maongezi ya wale wadada walioonekana kuzoeana kwa muda mrefu kidogo sababu walikuwa wanapiga story huku wakicheka
“Hivi Alex ni raia wa nchi gani?”mmoja aliuliza
“nasikia ni mtanzania”Alijibu mwenzake huku akiwa hana uhakika
Cindelela alishtuka sana kusikia kwamba Alex ni raia wa Tanzania,alianza kujiuliza maswali mengi sana bila kupata jibu sababu hakuamini kama kuna mtanzania ambaye angeweza kusumbua vichwa vya wenyeji kama Alex ananchofanya kwa kipindi icho
“Huyu Alex ni nani?kumbe watanzania nao ni maarufu katika nchi za ulaya?natamani sana nimuone Alex ili tujenge urafiki sababu siwezi kuwa mpweke wakati kuna mtanzania mwenzangu”Cindelela alikuwa anajiuliza bila kupata jibu
Mwisho aliamua kufikia uamuzi wa kumtafuta Alex ili wawe marafiki sababu walikuwa wanatokea katika nchi moja.Kiu yake ya kumjua Alex iliendelea kufika kooni na kujikuta akitaka kuwaongeresha kitu wale wadada lakini alikuwa anasita sababu bado alikuwa ni mgeni.Mdomo wake ulikuwa unachezacheza lakini alikuwa aongei kitu chochote sabau alikuwa anaogopa kuwauliza
Cindelela aliamua kupuuzia kwanza ili akizoea mazingira ya hapo chuoni ndiyo aanze mchakato wa kumtafuta Alex ili waunde urafiki.Laiti kama angejua Alex ni yule kijana aliyemdharau Tanzania sidhani kama angekuwa hata na hiyo hamu ya kumtafuta
Siku nazo ziliendelea kusogea huku Cindelela akianza kuyazoea mazingira ya hapo chuoni.Kwa uzuri aliokuwa nao wanaume nao walianza kumfukuzia kwa kasi huku wengi wao wakiambulia patupu sababu Cindelela bado alikuwa na msimamo wake.Sifa zake zilianza kusambaa kila upande wa hapo chuoni sababu alikuwa ni miongoni mwa wasichana wazuri tena kutoka katika bara la Afrika
Cindelela alikuwa anatumia jina lingine ili kuwadanganya wanaume hapo chuoni sababu alikuwa hataki jina lake lifahamike kwa watu.Cindelela alikuwa anatumia jina la Aliciana au kwa kifupi Alice na kufanya Jina ilo lifanane kidogo na jina la Alex.Jina la Alice na uzuri wake ulikuwa gumzo kwenye darasa lao na kwenye sehemu mbalimbali za hapo chuoni kitu kilichomfanya awe anajificha kuwakwepa wanaume wasumbufu na ving’ang’anizi
………………………………………………………………………………………………………………………………………
Kwa upande wa Alex hakujua kitu chochote juu ya ujio wa Cindelela katika chuo icho zaidi ya kusikia sifa kuhusu Alice.Sifa za Alice zilimfikia Alex kutoka kwa rafiki yake wa karibu ambaye alikuwa anamsaidia katika kampeni zake za kugombea Uraisi wa chuo
“Alex umemuona msichana mrembo Alice?”Rafiki yake alimuuliza siku moja wakiwa wanapata chakula cha mchana
“hapana sijamuona zaidi ya kusikia sifa zake kwa mbali”alisema Alex
“Alex kiukweli Alice ni mzuri sana na katika hiki chuo cha Birmingham nadhani atasumbua sana sababu ana sifa za kipekee”Alisema rafiki yake
“Sidhani kama anafikia sifa za Cindelela”alisema Alex
“Cindelela ndiyo nani?”aliuliza rafiki yake anayejulikana kwa jina la John raia wa Ubeligiji
“Cindelela ndiyo msichana ambaye nimetokea kumpenda kuliko wasichana wote katika ulimwengu huu,na kama siku akatokea msichana mwingine ambaye ataiteka akili yangu basi atakuwa ameniondoa kwenye mateso mazito sana juu ya Cindelela sababu nateseka sana kwaajili yake”Alex alisema kwa kirefu
“kwani huyo Cindelela yupoje?”John aliuliza
“John siku ukimuona Cindelela hata huyo Alice unayesema ni mzuri nadhani utamuona ni kituko,Cindelela amekamilika pande zote kwani ni mzuri kupindukia kuanzia sura mpaka umbo lake.Kwa mara ya kwanza niliyomuona mwili wangu ulikufa ganzi na kujikuta kama nimepigwa na shoti katika mwili wangu.Mpaka sasa ninapoongea na wewe Nampenda sana Cindelela japo najua yupo mbali na mimi sababu nimemuacha Tanzania”Alex alisema kwa hisia na kufanya machozi kidogo yamdondoke
“Alex unanifanya na mimi niwe na hamu ya kumjua huyo Cindelela sababu kwa uzuri aliokuwa nao Alice arafu wewe unasema hawezi kumfikia huyo Cindelela basi itakuwa ni balaa”alisema John
“ningekuwa na simu yangu hapa ningekuonyesha picha yake kwenye mtandao wa facebook”Alisema Alex
Walipiga story nyingi sana mpaka walipomaliza kula chakula.Alex nae alikuwa na hamu ya kumuona huyo Alice baada ya kusikia anatoka katika nchi ya Tanzania.Kwakuwa kipindi icho alikuwa kwenye hatua za mwisho wa kampeni aliamua kusubiri mpaka uchaguzi utakapopita ndio aanze mchakato wa kumtafuta Alice ili amuone
Kabla hata uchaguzi mkuu haujaanza timu ya Birmingham ilikuwa inatakiwa kucheza na timu ngumu ya Middlesbrough,Alex nae alitakiwa kucheza mechi hiyo sababu alikuwa kwenye mipango ya kocha.Alex alifika kambini na kuanza maandalizi kwaajili ya mechi hiyo ambayo ilikuwa uinachezewa katika uwanja wa St Andrew’s ambao ni uwanja wa nyumbani.siku mija kabla ya mechi Alex alichukua T shirt nyeupe na kuanza kuandika maandishi ambayo wenzake hawakuyaelewa hata kidogo sababu aliandika kwa lugha ya Kiswahili
Siku ya mechi ilipofika kila mtu aliingia uwanjani kwa dhumuni la kuangalia mechi hiyo ambayo ilionekana kuwa na upinzani mkubwa sana sababu timu zote zilikuwa na nia ya kupanda daraja.Timu ziliingia uwanjani na kila mtu alikuwa na presha ya hali ya juu sababu wote walikuwa wanataka ushindi ili kupata nafasi ya kuelekea daraja la juu
Mechi ilianza kwa utulivu huku kila mmoja akijihami asije akafungwa mapema na kupoteza ule mchezo.Alex alikuwa anaonyesha cheche zake lakini mabeki walionekana kumkamia sababu walikuwa wanamchezea rafu na kusababisha faulo za hapa na pale japo hazikuzaa mabao.Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao hata moja
Timu zilienda mapumziko bila timu yoyote kupata bao na kufanya uwanja uwe kimya kwa muda mrefu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu zikiwa zinashambuliana kwa zamu lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata goli.Alex roho ilikuwa inamuuma sana sababu kuna kitu alikusudia kukifanya lakini aliona kama inashindikana sababu hajafanikiwa kupata goli lolote
Dakika moja kabla ya mpira kuisha Alex alipata pasi nzuri kutoka upande wa kulia na kuanza kuingia na mpira kwa kasi huku akipiga chenga mabeki na kupiga shuti kali sana kwa mguu wake wa kulia.Shuti ilo liliingia moja kwa moja wavuni na kufanya Alex awe ameipatia timu yake bao la kuongoza ambalo liliwanyong’onyesha mashabiki wa timu pinzani
Baada ya kufunga goli Alex alikimbilia upande wa waandishi wa habari na kuvua jezi yake na kubaki na t shirt nyeupe iliyoandikwa”NAKUPENDA CINDELELA”.Japo alipewa kadi ya njano lakini dhumuni lake lilikuwa tayari limeshatimia.Mpira ulimalizika na timu yao ikapata ushindi wa bao moja kwa sifuri
Kwa ushindi hule kila mtu ndani ya club hiyo alifurahia sababu aliona ndoto ya kupanda ligi kuu imekaribia,Kelele zilikuwa zinasikika kwenye nchumba cha kubadilishia nguo huku washezaji wakimwagiana maji na kucheka kwa furaha.Baadhi walimfuata Alex na kumuuliza kwenye ile Tshirt alikuwa ameandika nini sababu walikuwa hawajaelewa kitu chochote
“kwasasa hampaswi kujua ila kama waandishi wa habari wakiniita nizungumzie nadhani nitaongea kwa kirefu sana kuhusu yale maneno”Alex aliwaambia wachezaji wenzake
Kesho yake vyombo vyote vya habari vilikuwa vinatangaza kuhusu yale maandishi yaliyoandikwa kwenye T shrt aliyoivaaa Alex.Kila mtu alikuwa anazungumza lake sababu walikuwa hawajaelewa anamaanisha nini.Wapo waliodhani kwamba yale maneno yanahusu upingaji wa ubaguzi wa rangi na wengine wakiwaza wanavyojua wao wenyewe
Cindelela hakuwa mfuatiliaji wa mpira lakini alifanikiwa kuona kidogo ile tshirt akiwa anaangalia taarifa ya habari ya siku hiyo.Japo hawakuonyesha sura ya huyo mchezaji lakini yale maneno yalimfanya ashtuke sana sababu ile Tshirt ilikuwa imeandikwa jina lake Tena ni kwa maneno ya Kiswahili.Mapigo ya moyo wake yalianza kwenda mbio kwani alikuwa na hamu ya kujua ni nani aliyeandika maneno yale tena kwa Kiswahili
“ni nani huyu aliyeandika maneno haya wakati mimi sijawahi kumtajia mtu yoyote jina langu ili?”Cindelela alijiuliza mwenyewe na kukosa jibu la moja kwa moja
Kwa kipindi hicho Cindelela alikuwa na hamu mbili,kwanza ni kumjua Alex ambaye anaonekana ni mtanzania maarufu sana hapo chuoni,hamu ya pili ni kujua nani aliyeandika yale maneno kwenye jezi yake.Kichwa kilikuwa kinamuuma sababu sababu lile jina hakuwahi kumtajia mtu yoyote pale chuoni
“mh isije kuwa naumiza kichwa wakati kuna Cindelela mwingine hapa jijini”Cindelela alijisemea mwenyewe
Aliamua kupuuzia yale maneno na kuamua kulifuatilia jambo moja tu ambalo lilikuwa kuhusu Alex.Aliapa kwamba lazima amtafute Alex ili wajenge urafiki sababu alikuwa mtanzania mwenzake anayesoma katika chuo icho.Harakati za kumtafuta Alex zilianza ksababu kipindi cha uchaguzi nacho kilikuwa kimekaribia kwahiyo Alex alikuwa kwenye pilika nyingi sana
Siku ya uchaguzi ilifika na watu wote wakawa wanapiga kura kumchagua raisi wa chuo,miongoni mwa hao wanafunzi alikuwepo Cindelela ambaye alimchagua Alex bila hata ya kumjua sura yake.Uchaguzi uliisha salama na matokeo yalihaidiwa kutangazwa kesho yake sababu muda ulikuwa umeenda sana
“kesho ndiyo tutatangaza matokea na kumsimamisha mtu ambaye ameshinda kuwapa shukrani zake kwenu”alisema mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi
Kila mtu alikuwa anashahuku ya kujua nani atashinda kiti cha uraisi wa chuo japo wengi walishajua kwamba Alex lazima aibuke kidedea.Hata Cindelela mwenyewe alikuwa na hamua ya kutaka kumuona huyo Alex akisimama ili kutoa shukrani sababu alikuwa na asilimia mia moja ya kushinda ule uchaguzi
Masaa nayo hayakukawia kwani siku ya kutangazwa mshindi ilifika na watu wote walikusanyika sehemu moja kwaajili ya kujua ni nani aliyeshinda huo uchaguzi.Alex hakuwa na wasiwasi sana sababu kila mtu alikuwa anampa moyo kwamba mshindi ni yeye kutokana na kuwa kipenzi cha watu wengi sana
Cindelela nae alikuwa njiani kusikiliza kama Alex ameshinda ili amuone sura yake sababu kwa kipindi hicho mababngo yote yalikuwa hayapo bali kulikuwa na makaratasi ambayo hayakuwa na picha,kwa mbali alisikia sauti ya kuwa Alex ndiyo mshindi wa kiti cha uraisi wa chuo
Cindelela aliongeza speed ili kuwahi pale kwenye mkusanyiko wa watu ili amuone Alex akiongea na wanafunzi.Wakati akitembea alijikuta akidondoka chini kisha akapoteza fahamu na tatizo alikujulikana ni nini.Watu waligeuka na kumbeba juu juu ili kumkimbiza hospitali sababu alionekana na hali mbaya sana
Gari la wagonjwa lilifika na kumpakiza Cindelela kwenye hospitali ya chuo ili apate huduma ya kwanza na kama ikishindikana wampeleke hospitali kubwa.Wanafunzi wote walikuwa wamehamaki sababu lile tukio lilitokea kwa haraka sana na ukicheki Cindelela alikuwa ameshapata umaharufu kutokana na urembo aliokuwa nao
Alex alikuwa hajui kama Cindelela ndiyo ameanguka pale sababu wanafunzi wengi walikuwa wanataja jina la Alice.Baada ya Cindelela kuwaishwa hospitali Alex alisimama tena kwenye jukwaa na kuanza kuzungumza maneno machache kwaajili ya shukrani kwa watu waliompigia kula na kumfanya awe mshindi wa kiti cha uraisi hapo chuoni
“Napenda kumshukuru mungu kwa kunifanya nipate heshima hii kubwa hapa chuoni,pia nawashukuru wanafunzi wenzangu wote mlioweza kunichagua sababu bila ya ninyi nisingesimama mahali hapa.Nadhani tutashirikiana katika kila jambo ili kufanya maendeleo katika chuo chetu.asanteni sana”Alex alisema maneno machache sana lakini yalipokelewa na makofi yaliyopigwa kwa dakika nzima bila kupumzika
Alex alimaliza kuongea na wanafunzi wote walitawanyika ili wakaendelee na shughuli nyingine za kimasomo.Alex alikuwa amesimama na rafiki yake John wakiongea maneno machache huku kwa mbali lilionekana kundi la wanafunzi likiwa linamsubiri Alex ili wazungumze nae
“Alex yule dada aliyeanguka ndiyo Alice niliyekuwa nakuambia siku zile”alisema John rafiki wa Alex
“mimi sijamuangalia vizuri sababu nilikuwa nimeconcentrate sana na huku mbele na ndiyo maana sikumuona huyo mwanamke aliyedondoka”Alex alisema
“Basi hyuyo aliyedondoka ndiyo Alice msichana mrembo aliyepata umaarufu kwa kipindi kifupi tu tangu aingie huku chuoni”Alisema John
“Basi ngoja niende hospitali nikamuangalie huyo Alice unayemsemea tena kwakuwa ni mtanzania mwenzangu nadhani itakuwa vizuri nikifahamiana nae”alisema Alex huku akianza kuondoka
Alex aliongozana na John kuelekea hospitali ya chuo ili kumuona Alice kama anavyofahamika na watu wengi lakini kwa jina halisi anaitwa Cindelela.Walifika ndani ya hospitali ya chuo na kuelekezwa wapi alipofikishwa mgonjwa,moja kwa moja Ale alianza kuelekea kwenye wodi aliyolazwa Cindelela
“Naomba mniambie mgonjwa aliyedondoka kwenye mkutano yupo wapi?”alex aliwauliza wauguzi waliokuwa karibu yake
“yupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi,kwani wewe ni nani yake?”muuguzi mmoja aliuliza
“mimi ni mwenzake kutoka Tanzania”Alex alisema kwa kujiamini bila kujua ni nani aliyedondoka
“okey ngoja tuongee na daktari”Muuguzi alisema na kuelekea ofisini kwa daktari
Baada ya muda kidogo alionwekana muuguzi akiwa ameongozana na mtu aliyevaa koti jeupe.Alikuwa ni daktari ambaye anausika na yule mgonjwa aliyedondoka pale chuoni
“habari yako kijana”dokta alimsalimia Alex
“salama daktari nimekuja kumuona mgonjwa aliyeletwa sasa hivi”Alex alisema
“wewe ni ndugu yake”daktari aliuliza
“Mimi siyo ndugu yake ila ni mtanzania mwenzake na ukicheki tunasoma kwenye chuo kimoja”Alex alisema kwa umakini
“nifuate ofisini”Daktari alisema na kuanza kuelekea ndani ya ofisi
Walifika kwenye ofisi na daktari alikaa kwenye kiti ili aanze kumuambia Alex kuhusu hali ya mgonjwa ilivyo.Alex nae alikuwa maini sana kumsikiliza Daktari anasemaje
“Mgonjwa yupo kwenye hali mbaya sana na tumeshawasiliana na wazazi wake wametuambia kuanzia kesho watakuwa hapa ila kuna baba yake mdogo ni mwalimu katika chuo chenu ndiyo anafuatilia kila kitu hapa”Daktari alisema
“kwani tatizo ni nini?”Alex aliuliza
“mgonjwa wenu ana tatizo la figo lakini kilichomuangusha ni blood pressure,kwa sasa tunafanya mpango wa kumuhamisha hapa na kumpeleka kwenye hospitali ya st Thomas iliyopo London ili akapate huduma ya hali ya juu kutoka kwa madaktari bingwa”alisema Daktari
“naweza kumuona mgonjwa?”Alex aliuliza
“kwasasa haiwezekani sababu bado anapewa huduma ya kwanza kabla hatujampeleka huko”alisema daktari
“basi mimi nitasubiri nje mpaka mtakaponiruhusu nimuone”Alex alisema kisha akatoka na kwenda kukaa sehemu ya kusubiria wagonjwa
Alex hakujua ni kitu gain kilichomsukuma mpaka kukaa nje kusubiri aitwe akamuone mgonjwa wakati mgonjwa mwenyewe alikuwa hata amjui kwa sura zaidi ya kusikia jina la Alice.Alex alitamni kuondoka ili arudi baadae sababu alikuwa amechoka sana kusubiri,,kila alipotaka kuondoka kuna sauti ilikuwa inamuambia kwamba asiondoke sababu ampendae yupo mule ndani
“Alex usiondoke hapo ulipo sababu utakosa kumuona yule unayempenda”sauti ya kwanza ilikuwa inasema kwenye akili chake
“Alex ondoka bwana hakuna kitu chochote utakachokipata hapo sababu huyo mtu haumfahamu hata kidogo sasa ya nini kupoteza muda”sauti ya pili ilikuwa inasema ndani ya kichwa chake
Sauti hizo mbili zilimfanya Alex achanganyikiwe sababu alikuwa hajui aifuate sauti gain kwani zote zilikuwa na maana yake.Alex alikuwa anasimama na kuzunguka zunguka ili kupoteza muda kidogo kwani alikuwa na hamu sana ya kumuona mgonjwa sabau alikuwa ni mtanzania mwenzake.Kwa wakati huo rafiki yake John hakuwa maeneo yale sababu kuna vitu vyake alienda kufuatilia
Alex baada ya kusubiri kwa muda mrefu aliamua kuondoka kidogo ili baadae harudi kumuangalia mgonjwa.Tukio la Alex kuondoka tu dakika tano baadae helikoptaya msalaba mwekundu ilitua kwenye hiyo hospitali na moja kwa moja mgonjwa alipakiwa huku akiwa na madaktari wawili na muuguzi mmoja.Ile safari ilikuwa ni kuelekea kwenye hospitali ya St Thomas kwaajili ya uchunguzi zaidi sababu mgonjwa hakuonekana kupata nafuu japo alipewa huduma ya kwanza kwenye hospitali ya chuo
Alex alikuja kurudi baadae na kuuliza kama anaweza kumuona mgonjwa,Jibu alilolipata lilimkatisha tama sababu hakutegemea kama ataambiwa kwamba mgonjwa ameshaondolewa pale na kupelekwa hospitali nyingine,Alex alitoka pale mapokezi na kwenda kukaa kwenye kiti ili apange kama anaweza kwenda kwenye hospitali ya St Thomas akamuone huyo mgonjwa
“hivi kwanini nasumbuka hivi kwa mtu ambae simfahamu?hivi ingekuwa ndo Cindelela amedondoka si ningekufa na mimi?lakini kwakuwa huyo aliyedondoka ni mtanzania mwenzangu acha nikamuone”Alex alijisemea na kuondoka zake kuelekea kwake ili akapange safari ya kuelekea huko alipopelekwa mgonjwa
…………………………………………………………………………………………………………………….
Cindelela baada ya kufikishwa kwenye hospitali ya St Thomas haraka haraka matibabu yakaanza kufanyika ili kunusuru maisha yake sababu alionekana kwenye hali mbaya sana,Miguu ilionekana kuvimba huku mwili wake ukiwa unataka kubadilika Rangi,alikuwa anahenma kwa msaada wa kifaa cha oxygen kilichowekwa kwenye pua yake
“mgonjwa inatakakiwa apatiwe figo haraka sana kabla hatujampoteza”alisema daktari mmoja
“tutapata wapi hiyo figo?aliuliza daktari mwingine
“hata kama ni kwa hela hiyo figo inatakiwa kupatiokana la sivyo huyu mgonjwa hawezi kufika siku mbili”alisema Daktari mkuu
“tusubiri wazazi wake waje ili kama inawezekana watoe figo kwaajili ya kumsaidia mtoto wao”alisema daktari mwingine Muhafaka ulifika na kila daktari aliekea kwenye ofisi yake ili kuandaa mipango ya kumfanyia upasuaji
Ndege aliyoipanda mzee Jacobo na mkewe ilifika nchini Uingereza na moja kwa moja aliingizwa kwenye helikopta iliyompeleka kwenye hospitali ya St Thomas ili akamuone binti yake aliyekuwa kwenye hali mbaya sana.Haikuchukua muda mrefu wakawa wameshafika nje ya hospitali hiyo
Mzee Jacobo alikuwa anatokwa na machozi japo alikuwa anajikaza kiume lakini kwa mkewe machozi yalishamkauka sababu alilia kupitiliza.Cindelela ndiyo alikuwa ni mtoto wao pekee na hawakuwa na uwezo tena wa kupata mtoto mwingine na kama ikitokea Cindelela amepoteza maisha watabaki bila mtoto
“Dokta naomba uniambie kama mwanangu ni mzima”mzee Jacobo alisema huku machozi yakimtoka
“mwanao ni mzima lakini inahitajika figo kwa haraka sana lasivyo tunaweza kumpoteza”Daktari alisema
“sijui tutafanyaje daktari sababu mimi hapa nilipo nimeshafanyiwa upasuaji sababu nilipata ajali na mke wangu nae anatatizo la figo lakini alshapatiwa tayari sasa sijui mwanangu nitamsaidiaje” mzee Jacobo alilalama
“basi inatakiwa tununue kwa mtu ambae yupo tayari kutoa”alisema daktari
“kwa gharama yoyote mtafuteni huyo mtu mimi nitalipa gharama zote”alisema mzee Jacobo
“sawa nenda kapumzike tufanye utaratibu wa kumpata huyo mtu daktari alisema
Mzee Jacobo na mkewe walitoka pale hospitali na kupelekwa hotelini kwaajili ya kupumzika ili mtoto wao aendelee na huduma
……………………………………………………………………………………………………..
Kwa upande waAlex alikuwa kama amechanganyikiwa sababu alikuwa hajielewi kutokana na sauti iliyokuwa inamuimiza aende jiji la London ili akaangalie hali ya mgonjwa inavyoendelea.Aliamua kwenda kwenye uongozi wa timu ili aombe ruhusa ya kwenda kumuona mgonjwa .Kutokana na kipindi hicho kilikuwa cha mapumziko uongozi wa timu ulimruhusu aende lakini asije akachelewa sabna sababu anatakiwa aanze mazoezi siku siyo nyingi
Alex alipanga safari haraka haraka sana na mchana wake baada ya kuomba ruhusa alielekea kwenye uwanja wa ndege ili asafiri kuelekea jijini London kwaajili ya kwenda kumuangalia mgonjwa.Alex alijishangaa sana kwani machozi yalikuwa yanatoka yenyewe bila hata ya kufabnya kitu chochote kile
“kwakuwa ni mtanzania mwenzangu ndiyo maana nasumbuka sana na ukicheki mimi ni kiongozi wa pale chuoni nahitajika kuonyesha mfano kwa wanafunzi wenzangu”alijisemea Alex
Ndege ilitua kwenye jiji la London na moja kwa moja Alex alichukua Tax iliyompeleka kwenye hospitali ya St Thomas ili akaangalie hali ya Alice inaendeleaje.Alex aliingia ndani ya hospitakli hiyo na kupelekwa kwenye ofisi ya Daktari kwaajili ya kupata maelekezo
“samahani sana daktari nimekuja kumuangalia mgonjwa anayetiokea kwenye chuo cha Birmingham”Alisema Alex baada ya kuingia kwenye chumba cha Daktari
“mh ni ngumu sana kumuona sababu yupo kwenye hali mbaya sana na ukicheki inahitajika figo ya haeraka sana kwaajili ya kusaidia huyo mgoinjwa”Dokta alisema
“dokta me naomba nimuone naweza nikajitolea figo yangu kwaajili yake”Alex alijikuta ameropoka bila hata kutegemea na kumfanya yule dokta atabasamu
“kijana utakuwa umetusaidia sana na kuna zawdi kubwa sana itatolewa kwaajili yako”alesema Daktarii
“Naomba nimuone mgonjwa kwanza”Alex alisema
“okey twende ukamuone”Daktari alisema huku akisimama
Alex nae aliinuka na safari ya kuelekea alipolazwa Cindelela ikaanza,Alex alijikuta mwili wake ukitetemeka huku jasho likimtoka mpaka mwenyewe akawa anajishangaa kwanini kitu kama kile kinatokea.Daktari alishika mlango wa cghumba special alicholazwa Cindelela kwaajili ya kuufungua ili waingie ndani
ITAENDELEA

No comments:
Post a Comment